Audio & Video

Halmashauri mkoani Mwanza zatakiwa kubuni vyanzo vipya vya mapato

on

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Halmashauri zote mkoani Mwanza zimetakiwa kubuni vyanzo vipya vya ukusanyaji wa mapato ikiwemo kurekebisha sheria ndogo zinazotoa mwanya kwa baadhi ya wafanyabiashara kukwepa kulipa kodi na tozo mbalimbali.

Mkuu wa wilaya ya Sengerema Mwal.Emmanuel Kipole alitoa rai hiyo jana Mei 30, 2018 kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, wakati akifungua mkutano wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa Tanzania ALAT tawi la mkoa wa Mwanza uliofanyika wilayani humo.

Mwl. Kipole alisema halmashauri hazipaswi kulalamika kukosa vyanzo vya mapato ikiwemo kodi ya majengo baada ya kuhamishiwa Serikali Kuu, badala yake zinapaswa kubuni vyanzo vipya vya mapato.

“Zipo sheria ndogo ndogo zinazojaribu kutoka unafuu usio wa lazima kwa wafanyabiashara wa mazao ya samaki kwa kutoa kiwango cha ujumla cha ushuru na hivyo kuzikosesha halmashauri mapato wakati Sheria mama Uvuvi ya mwaka 2003 pamoja na kanuni zake za mwaka 2009 inaweka viwango vya tozo ya ushuru kwa asilimia ama kiasi cha mzigo”. Alisema Mwl.Kipole.

Naye Mwenyekiti wa ALAT mkoani Mwanza Hilal Elisha alizitaka halmashauri mkoani Mwanza kubuni na kusimamia vyema miradi mbalimbali ya maendeleo kwa kuwashirikisha wananchi, ambapo alitoa pongezi kwa halmashauri ya Sengerema kwa kutekeleza vyema miradi yake ikiwemo afya, elimu pamoja na maji.

Katika hatua nyingine mkutano wa ALAT mkoani Mwanza ulimzawadia cheti pamoja na fedha shilingi laki mbili Mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa ya Ilemela John Wanga kwa kuhudhuria mikutano yote ya jumuiya hiyo ambapo Wanga alielekeza fedha hizo zinunue mchele kilo 200 kwa ajili ya wanafunzi wa shule maalum za msingi Itumbili wilayani Magu na Mitindo wilayani Misungwi.

Pia mkutano huo ulitoa shilingi milioni mbili ili kusadia ujenzi wa bweni la wasichana katika shule ya sekondari Nyamatongo halmashauri ya Sengerema, linalojengwa kwa nguvu za wananchi, halmashauri pamoja na wadau wa maendeleo.

Mkuu wa wilaya ya Nyamagana, Mwl.Emmanuel Kipole akifungua mkutano wa ALAT tawi la mkoa wa Mwanza uliofanyika wilayani humo.

Mwenyekiti wa ALAT mkoani Mwanza, Hilal Elisha akizungumza kwenye mkutano huo.

Mkutano wa ALAT tawi la mkoa wa Mwanza ulifanyika jana wilayani Sengerema ukitanguliwa na ziara ya kamati tendaji ya jumuiya hiyo iliyolenga kukagua miradi ya maendeleo.

Katibu wa Jumuiya ya ALAT tawi la Mwanza Chrispin Luanda, akizungumza kwenye mkutano huo.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela ambaye pia ni mjumbe wa jumuiya ya ALAT mkoani Mwanza akitoa neno la shukurani baada ya ufunguzi wa mkutano huo.

Mwenyekiti wa ALAT mkoani Mwanza Hilal Elisha (wa pili kushoto), akimkabidhi hundi ya shilingi laki mbili Mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa ya Ilemela John Wanga (wa pili kulia) baada ya kuhudhuria vikao vyote vya jumuiya hiyo.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela John Wanga (kushoto), akimkabidhi fedha mwenyekiti wa halmashauri ya Misungwi Antony Bahebe (kulia) ili kununua mchele kilo 100 kwa ajili ya wanafunzi wa shule maalum ya msingi Mitindo. 

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela John Wanga (wa tatu kushoto), akimkabidhi fedha Mkurugenzi wa halmashauri ya Misungwi Eliurd Mwaiteleke (kulia) ili kununua mchele kilo 100 kwa ajili ya wanafunzi wa shule maalum ya msingi Mitindo. 

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela John Wanga (kushoto), akimkabidhi fedha Mkurugenzi wa halmashauri ya Magu Lutengano Mwalwiba (kulia) ili kununua mchele kilo 100 kwa ajili ya wanafunzi wa shule maalum ya msingi Itumbili.

Baadhi ya wajumbe wa mkutano wa ALAT mkoani Mwanza wakifuatilia mkutano uliofanyika wilayani Sengerema.

Wakishiriki wa mkutano wa ALAT mkoani Mwanza akiwemo Naibu Meya halmashauri ya Jiji la Mwanza Bhiku Kotecha (katikati).

Baadhi ya wajumbe wa mkutano wa ALAT mkoani Mwanza wakifuatilia mkutano uliofanyika wilayani Sengerema.

Wajumbe wa Kamati Tendaji ya ALAT mkoani Mwanza.

Tazama BMG Online TV hapa chini 

ISOME PIA HABARI HII UFAFANUZI: Mwenyekiti wa ALAT mkoa wa Mwanza

Recommended for you