Habari Picha

Waalimu Shinyanga wapigwa msasa na Chuo Kikuu Huria Tanzania

on

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mheshimiwa Josephine Matiro amefungua warsha maalumu kwa walimu wa shule za msingi na sekondari zilizopo katika manispaa ya Shinyanga kwa ajili ya kuwajengea uelewa kuhusu masuala ya jinsia.

Kadama Malunde, Malunde 1 Blog

Warsha hiyo iliyoandaliwa na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania tawi la Shinyanga kwa ufadhili wa benki ya CRDB tawi la Shinyanga imefanyika leo Jumatatu Mei 14,2018 katika chuo hicho mjini Shinyanga kwa kukutanisha walimu 100.

Warsha hiyo ni sehemu ya Mpango Maalumu uliobuniwa na Chuo hicho kwa ajili ya kujenga uwezo watumishi wa umma hasa walimu juu ya masuala ya jinsia.

Akifungua warsha hiyo,Matiro alisema mbinu stahiki za kupambana na ukatili wa kijinsia zitafanikiwa endapo dhana,aina,matokeo na sababu za ukatili zitaeleweka kuanzia ngazi ya msingi hususani shuleni ambapo watoto wanatumia muda mwingi wa maisha yao.

“Niwapongeze sana kwa kuanzisha mpango huu wa kuwafikia walimu,warsha hii ni nyeti sana na huenda kuna walimu ambao walishawahi kushuhudia ama kutenda vitendo vya kibaguzi kwa watoto kwa kujua ama kutojua,kwa hali hii vitendo hivyo vina athari kubwa katika maendeleo ya kitaaluma kwa watoto”,alisema Matiro.

Aidha alisema ni jukumu la walimu na shule kuweka kanuni na taratibu ambazo zitatoa ulinzi na kusaidia jamii nzima ya shule kuishi kwa amani na kuzingatia usawa.

“Niwaombe msiishie kwa walimu pekee kutoa elimu hii,bali wafikieni pia watumishi wote wa umma kwani nao kwa sehemu yao wana mchango mkubwa katika ujenzi wa jamii inayothamini usawa wa kijinsia”,aliongeza.

Katika hatua nyingine aliishukuru benki ya CRDB kwa kuendelea kuwa wadau muhimu katika elimu na maendeleo katika jamii

Awali akizungumza,Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania,Kituo cha Shinyanga, Paschal Mheluka alisema lengo la warsha hiyo ni kuwajengea uelewa walimu kuhusu masuala ya jinsia ili wakawafundishe wanafunzi ambao watakuwa mabalozi katika jamii.

“Tumekutana na walimu 100 kutoka shule za msingi na sekondari za serikali na binafsi wanaofundisha somo la uraia kwani wanafundisha masuala mtambuka yanayohusu mambo ya jinsia”,alieleza.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mheshimiwa Josephine Matiro akizungumza wakati wa kufungua warsha maalumu kwa walimu wa shule za msingi na sekondari zilizopo katika manispaa ya Shinyanga iliyolenga kuwajengea uelewa kuhusu masuala ya jinsia.Mheshimiwa Josephine Matiro akizungumza wakati wa warsha hiyo.Kushoto ni Mratibu wa Masuala ya Jinsia katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania tawi la Shinyanga,Getrude Pastory Massawe ambaye pia Afisa Masoko wa chuo hicho.Kulia ni  Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania,Kituo cha Shinyanga, Paschal Mheluka.Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mheshimiwa Josephine Matiro akizungumza katika warsha hiyo na kueleza kuwa kukosekana kwa usawa baina ya wasichana na na wavulana shuleni na katika jamii ni chanzo kikuu cha ukatili kitu kinachofanya ukatili kuwa suala la kijinsia.Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania,Kituo cha Shinyanga, Paschal Mheluka akizungumza wakati wa warsha hiyo iliyokutanisha walimu 100 kutoka shule za msingi na sekondari zilizopo katika manispaa ya Shinyanga.Mratibu wa Masuala ya Jinsia katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania tawi la Shinyanga,Getrude Pastory Massawe ambaye pia Afisa Masoko wa chuo hicho akizungumza wakati wa warsha hiyo ambapo alisema wameamua kuanzisha mpango wa kutoa elimu ya masuala ya jinsia kwa walimu ili kuhakikisha walimu hao wanatoa elimu kwa wanafunzi wao kumaliza vitendo vya ukatili katika jamii.Washiriki wa warsha hiyo wakiwa ukumbini.Warsha inaendelea.Mwezeshaji wa masuala ya jinsia, Abubakar Rehani akiendelea kutoa mada ukumbini.Afisa Mikopo ya watumishi kutoka Benki ya CRDB tawi la Shinyanga,Lilian Kawamala akitoa mada kuhusu huduma zinazotolewa na benki hiyo ikiwemo mikopo kwa watumishi wa umma.

Washiriki wa warsha wakifuatilia mada ukumbini.

Walimu wakiwa ukumbini.Mwezeshaji wa masuala ya jinsia, Jumanne Mustapha akitoa mada kuhusu masuala ya jinsia.Washiriki wa warsha hiyo wakiwa wameshikana mikono ishara ya ushirikiano katika kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia katika jamii.Washiriki wa warsha hiyo wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro.Washiriki wa warsha hiyo wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro. ISOME PIA HABARI HII Shirika la AGAPE lawanoa wanafunzi mkoani Shinyanga 

Recommended for you