Habari Picha

WABUNGE WAZOZANA KUPINGA MAKAHABA KUONDOLEWE JIJINI.

on

Bunge la
nchini Kenya limepiga kura kuwaondoa makahaba katikati mwa mji mkuu Nairobi
nchini humo.
Waakilishi
katika bunge hilo walilazimika kupiga kura mara tatu ili kufikia maamuzi ya
kuwatimua makahaba mjini Nairobi. Kwa mara mbili matokeo ya kura yalikuwa sare,
lakini baada ya awamu ya tatu kura ya ndio ikashinda.
Hoja hiyo
iliwasilishwa na mwakilishi Bi Jane Mwasia, ikitaka wakuu wa jimbo kuwaondoa
makahaba mara moja kutoka katikati kwa jiji la Nairobi.Waakilishi wanaume
walipinga hoja hiyo mara tu ilipowasilishwa lakini mjadala ulipotokota, wengi
waliamua kupiga kura ya ndio wakati wengine wakijizuia.
Mjadala huo
nusura uzue makonde bungeni na kusababisha hisia mbalimbali miongoni mwa
waakilishi hao.Baadhi ya waakilishi hao walipendekeza kuwa sehemu maalum
itengewe makahaba hao baada ya wao kundolewa katika barabara zilizo katikati
mwa jiji.
“sina
tatizo na makahaba kwa sababu wengi wao hawana ajira. Kwa hivyo ni jukumu letu
kuwajengea sehemu ambako wataweza kuendeshea shughuli zao,” alisema mmoja wa
waakilishi hao.
Mwakilishi
mwingine, Manoah Mboko alisema kuwa suluhu kwa makahaba sio kuwaondoa mjini
bali ni kuwaoa kwani sheria ya kuoa zaidi ya mke mmoja ilipitishwa maajuzi.
Aliongeza kwamba makahaba wanachangia pakubwa sana katika uchumi wa mji wa
Nairobi.
Mwakilishi
mwingine alizua kicheko aliposema kuwa dunia nzima ni kama soko na hivyo kila
mtu aruhusiwe kuuuza bidhaa zake.
Na:bbcswahili