Audio & Video

Wachimbaji wadogo wa madini wamshangaza Naibu Waziri Biteko

on

Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko amewataka wachimbaji wadogo wa dhahabu katika machimbo ya Kunanga yaliyopo Bunda mkoani Mara kuhakikisha wanafanya shughuli zao kwa kuzingatia sheria ikiwemo kulipa mrahaba serikalini.

Biteko alitoa kauli hiyo alipofanya ziara katika machimbo hayo na kushangazwa na hatua ya wauzaji na wanunuzi wa madini katika mialo iliyo katika machimbo hayo kulipa takribani shilingi 250,000 kwa serikali ya Kijiji cha Kunanga lakini hakuna malipo yoyote yanayofanyika kwa halmashauri ama serikali kuu.

SOMA>>>BUNDA: Biteko atoa maamuzi sakata la mwekezaji kuwatimua wanakijiji

Recommended for you