Audio & Video

Wafanyakazi ATCL watakiwa kutanguliza uzalendo

on

Judith Ferdinand, BMG

Watendaji na wafanyakazi wa shirika la ndege nchini wametakiwa kufanya kazi kwa bidii na kwa uadilifu ili kutanua wigo wa utoaji huduma.

Mkuu wa wilaya Magu Mhe. Philemon Sengati ameyasema hayo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe. John Mongella kwenye jukwaa la biashara la ATCL lililofanyika Jijini Mwanza.

“Wafanyakazi wote kwa maana ya bodi, menejimenti mjitoe kwa moyo na kuchapa kazi kwa uzalendo, uaminifu, uhadilifu na kutoa huduma bora ili kampuni hii ipanuke na kuleta faida kwa taifa. Alisema Sengati.

Mkurugenzi Mkuu wa ATCL Mhandisi , Ladislaus Matindi  alisema serikali imeboresha huduma  na  kulifufua shirika hilo, ili kulifanya lifanye kazi kwa ufanisi, hivyo katika kuhakikisha wanazingatia hayo hawatoruhusu kutengeneza madeni ya serikali kwa viongozi wake kutumia huduma ya ndege hizo bila kulipa.

“Ili kuhakikisha shirika letu linafanya kazi kwa ufanisi na kuacha kutengeneza madeni ya serikali, kila kiongozi wake anayetumia usafiri wa ndege zetu lazima halipe na kwa hili sitakuwa na mzaha lazima tuwe na nidhamu mfano hivi karibuni  Rais Magufuli  alitumia ndege hizo katika safari zake  alilipa  na amezingatia utaratibu sasa kama mwenye mamlaka amethubutu je watendaji wake kwanini wasilipe”. Alisema Mhandisi Matindi.

Hata hivyo Meneja Mauzo na Usambazaji wa ATCL Edward Nkwabi alisema, kutokana na  idadi ya  ndege walizonazo kwa sasa, wameanzisha safari ya  kwenda Entebe (Uganda) na Bujumbura(Burundi) ambayo ilianza Agosti 2018 baada ya kupokea ndege mbili aina ya A220-300, wamepanga kuongeza safari ndani na nje ya nchi ikiwemo  Mpanda, Kahama, Iringa   pamoja na Mumbai nchini India),  malengo ya mbele wakipata ndege nyingine watapanua wigo hadi nchi za Afrika Magharibi, Ulaya na Amerika Kaskazini.

Mmoja wa washiriki wa jukwaa hilo, Eric Hamissi ambaye ni Kaimu Mkurugenzi Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) alisema shirika hilo linaleta mapinduzimakubwa katika usafiri wa anga hivyo alitumia fursa hiyo kuliomba kuanzisha safari za Mwanza hadi Dodoma ambako ndio makao makuu ya nchi yalipo kwani kwa sasa wanapata tabu  wakazi wa mikoa ya Kanda ya Ziwa kwani hadi wapitie Dar es salaam  na gharama inaongezeka.

SOMA Boeng 787-8 Dreamliner yaanza vyema safari zake ndani ya nchi

Recommended for you