Audio & Video

Wafanyakazi wa nyumbani wafunguka kwa hisia

on

Na George Binagi0GB Pazzo, BMG

Baadhi ya wafanyakazi wa nyumbani Jijini Mwanza wamefunguka kuhusu maisha yao huku pia wakilishukuru shirika la kutetea haki za watoto wafanyakazi wa nyumbani WoteSawa, kwa juhudi za kutetea haki na maslahi yao.

Wakizungumza kwa hisia kali kwenye kikao cha wadau wa kutetea haki za wafanyakazi wa nyumbani, walisema awali walikuwa wakinyanyaswa huku wakilipwa ujira kidogo lakini baada kuhudhuria semina za WoteSawa hali imebadilika.

Elisha Daud ambaye ni Afisa Programu kutoka shirika la WoteSawa anasema shirika hilo linatekeleza mradi wa uwezeshaji shirikishi kwa watoto wafanyakazi wa nyumbani Tanzania ili kuwajengea uwezo wafanyakazi wa nyumbani kutetea haki na maslahi yao sambamba na mafunzo mbalimbali ikiwemo saloni.

Baadhi ya wafanyakazi wa shirika la WoteSawa wakifurahia jambo baada ya kikao kilichofanyika Monarch Hotel Jijini Mwanza.

Elisha Daud ambaye ni Afisa Programu shirika la WoteSawa akifafanua jambo wakati wa kikao hicho.

Mikakati katika kikao hicho iliwekwa.

Mradi huu tayari umetoa mafunzo ya saloni kwa wafanyakazi wa nyumbani 17 Jijini Mwanza ili kuwajengea uwezo zaidi kiuchumi.

Baadhi ya wafanyakazi wa shirika la WoteSawa kama walivyonaswa na kamera ya BMG.

Kikao cha wadau wanaotetea haki za wafanyakazi wa nyumbani Jijini Mwanza kiliwashirikisha waajiri, wafanyakazi wa nyumbani, viongozi wa dini, wenyeviti wa serikali za mitaa pamoja na watendaji.

Kikao kikiendelea.

Washiriki walitoa maoni mbalimbali ili kwa pamoja kusaidia kuwatambua na kuwasaidia wafanyakazi wa nyumbani katika maeneo yao.

Washiriki walipendekeza kutumia mikutano ya mitaa pamoja na nyumba za ibada kuwatambua wafanyakazi wa nyumbani na kufuatilia haki na maslahi yao kama yanazingatiwa.

Waajiri wa wafanyakazi wa nyumbani wanahimizwa kuwapatia wafanyakazi wao mikataba ya ajira na kuwalipa stahiki zao kwa mjibu wa sheria kuanzia shilingi elfu 40 kwa mwezi.

Watoto chini ya umri wa miaka 14 hawaruhusiwi kuajiriwa na badala yake wapewe fursa ya kutimiza ndoto zao ikiwemo kupata elimu.

Wanajamii wanahimizwa kutoa taarifa ngazi husika ikiwemo serikali za mitaa pamoja na polisi pindi waonapo ukatili dhidi ya wafanyakazi wa nyumbani.

Baadhi ya washiriki wa kikao katika picha ya pamoja.

Tazama video hapa chini. 

ISOME PIA HABARI HII Juhudi za WoteSawa zaanza kuzaa matunda

Recommended for you