Audio & Video

RC Mwanza azindua Mpango wa Uwezeshaji Sekta Isiyo Rasmi kupitia NSSF

on

Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongeella akizungumza kwenye semina kwa wenyeviti wa vikundi vya wazalishaji mali mkoani Mwanza, iliyofanyika jana Juni 09, 2018 katika ukumbi wa JB Fairmont Hotel Jijini Mwanza.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongell amezindua rasmi Mpango wa Uwezeshaji Sekta Isiyo Rasmi, unaosimamiwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii NSSF na kuwahimiza wajasiriamali kujiunga kwenye vikundi ili kunufaika na mpango huo.

Mhe.Mongella alizindua mpango huo jana kupitia semina kwa wenyeviti wa vikundi vya wazalishaji mali (wajasiriamali) mkoani Mwanza, iliyolenga kuwajengea uwezo viongozi hao ili wakawahamasishe wanachama wao kujiunga na mfuko wa NSSF na kunufaika na huduma zinazotolewa na mfuko huo ikiwemo bima ya afya pamoja na fidia ya uzeeni.

Alisema mkoa wa Mwanza uko tayari kuhakikisha kila mwananchi anajiunga na hifadhi ya jamii ambapo aliwataka Wakurugenzi wa Halmashauri mkoani Mwanza kuwa wadhamini wakuu wa wajasiriamali huku wakisimamia vyema fedha za asilimia 10 zitolewazo kwa vijana, akina mama na walemavu ili ziwanufaishe wahusika.

Mwenyekiti wa Sekta isiyo Rasmi kutoka NSSF, Maryam Muhaji alisema viongozi wa vyama vya ujasiliamali mkoani Mwanza wameipokea vyema elimu iliyotolewa kwenye semina hiyo na kuonyesha utayari wa kujiunga na uanachama wa hiari wa mfuko wa NSSF ambapo benki za NMB na Azania tayari zimeonyesha nia ya kuwawezesha wajasiriamali ili kujiimarisha kiuchumi na kuendelea kunufaika na huduma za mfuko huo.

Mwenyekiti wa Sekta isiyo Rasmi kutoka NSSF, Maryam Muhaji akitoa ufafanuzi kuhusiana na semina hiyo.

Meneja wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii NSSF mkoani Mwanza, Matson Mwakila akitoa neno la shukurani baada ya RC Mongella kuzindua Mpango wa Uwezeshaji Sekta Isiyo Rasmi mkoani Mwanza unaosimamiwa na mfuko huo

Viongozi na washiriki mbalimbali wa semina hiyo

Mgeni rasmi RC Mongella, viongozi wa NSSF pamoja na washiriki wa semina wakiwa kwenye picha ya pamoja

Tazama BMG Online TV hapa chini 

SOMA Uzinduzi wa UMISSETA kitaifa mkoani Mwanza

Recommended for you