Habari Picha

WAJASIRIAMALI WAFUNDWA KUPITIA MAONYESHO YA NANE NANE 2017

on

Judith Ferdinand, Mwanza

Wajasirimali  mkoani Mwanza wamehimizwa kufuata utaratibu wa uzalishaji bidhaa zenye ubora na zinazokubalika na shirika la viwango Tanzania (TBS).

Wito huo ulitolewa jana na  Afisa Udhibiti na Ubora wa TBS mkoani humo, Ramadhan Hassan wakati akizungumza na BMG kwenye Maonyesho ya Nane Nane yanayofanyika kwa Kanda ya Ziwa kwenye uwanja wa Nyamuhongolo Jijini Mwanza.

Alisema kupitia maonyesho hayo wamewekwa karibu na wajasiriamali ambapo wanapata nafasi ya kutembelea mabanda yao na kuwaelekeza juu ya uzalishaji bora wa bidhaa, wapi wanapatikana pamoja na namna ya kufuata utaratibu zilizopo kisheria.

Alibainisha kwamba kuna baadhi ya viwanda pamoja na wajasiriamali  wanaozalisha bidhaa zilizo chini ya kiwango, hivyo TBS inajitahidi kuwapa semina ili waweze kuzalisha bidhaa zenye ubora ili wapate alama ya ubora kutoka shirika hilo itakayoswaaidia kupata wateja wengi.

“TBS tunajitahidi kudhibiti maeneo ya mipaka na bandari kwa ajili ya kupingana na wafanyabiashara ambao siyo waaminifu wanaoingiza bidhaa zisizo na ubora huku pia tukitembelea masokoni kukagua bidhaa hizo”. Alidokeza Hassan.

Kadhalika aliongeza kwamba kila mtu  anawajibu wa kutunza afya yake, hivyo mteja anatakiwa kutoa taarifa  ili sheria ifuate mkondo pindi aonapo sokoni bidhaa zilizopitwa na wakati.

Bonyeza BMG Habari, Pamoja Daima kuhusu Maonyesho ya Nane Nane 2017

Recommended for you