Audio & Video

Mkuu wa wilaya ya Misungwi awakabidhi wafugaji Ng’ombe wa kisasa

on

George Binagi-GB Pazzo @BMG

Mkuu wa Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, Juma Sweda amekabidhi madume tisa ya ng’ombe wa kisasa kwa wafugaji (wananchi) wa Kata za Misasi na Bujima kama mbegu kwa ajili ya kuwasaidia kuboresha mifugo yao.

Madume hayo yameboreshwa katika Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Mabuki na yameuzwa kwa wafugaji hao kwa bei ya ruzuku ya shilingi laki mbili kila mmoja ambapo gharama halisi ni kati ya shilingi laki sita hadi laki saba.

Akikabidhi madume hayo jana Mei 04, 2018, Sweda alisema lengo la serikali ni kuboresha maisha ya wananchi kwa kubadilisha mfumo wao wa maisha kwa kuwawezesha kujitegemea kiuchumi kupitia ufugaji wenye tija.

Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Misungwi, Eliurd Mwaiteleke alisema hatua hiyo ni mwanzo wa mikakati ya halmashauri hiyo kuanzisha kiwanda cha uchakataji maziwa kwani rasilimali maziwa ya kuendesha kiwanda hicho ipo na soko pia lipo.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Mabuki, Moses Ngendelo alisema lengo la kugawa madume hayo aina ya Nkole ni kuhakikisha wafugaji wanaboresha ufugaji wao kwa kufuga mifugo michache na yenye tija kupitia ufugaji wa ng’ombe wa maziwa pamoja na nyama.

Baadhi ya wafugaji waliopokea madume hayo walishukuru kwa fursa hiyo na kuahidi kuyatunza vizuri kwa ajili ya manufaa yao pamoja na ya wafugaji wengine na kwamba wamejifunza kushughulika na ufugaji wa kisasa na wenye tija.

Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Mabuki, Moses Ngendelo, akitoa ufafanuzi kuhusiana na zoezi hilo la kuwakabidhi wafugaji madume ya ng’ombe.

Mwenyekiti wa halmashauri ya Misungwi, Antony Baheme kwenye zoezi hilo.

Mkuu wa wilaya Misungwi, Juma Sweda pamoja na viongozi wa halmashauri ya Misungwi walipokuwa katika ofisi za taasisi ya Utafiti wa Mifugo Mabuki.

Mkurugenzi halmashauri ya Misungwi, Eliurd Mwaiteleke (kushoto) akifuatilia jambo kwa makini. Kulia ni Afisa Mifugo na Uvuvi wilayani Misungwi, Dkt.Chrispine Shami.

Mwenyekiti wa halmashauri ya Misungwi, Antony Baheme (kulia) pamoja na Makamu wake Nicodemus Ihano.

Baadhi ya watumishi wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Mabuki.

Bonyeza HAPA Kikao cha Baraza la Madiwani Halmashauri ya Misungwi.

Recommended for you