Audio & Video

WANA CCM MWANZA WACHAGUA MAJEMBE YA KAZI

on

Chaguzi ndani ya Chama cha Mapinduzi zimezidi kupamba moto kwenye Kata mbalimbali katika Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, ambapo jana CCM Kata ya Pamba walifanya uchaguzi wa kuwapa viongozi wake.

Katika uchaguzi huo uliofanyika juzi Agosti 04,2017, Ayoub Michael Oyugi alichaguliwa kuwa Mwenyekiti, Augustine Bwire akachaguliwa kuwa Katibu huku Laurent Ryoba Kohe akichaguliwa kuwa Katibu wa Siasa na Uenezi.

Waliochaguliwa kuwa wajumbe wa kamati ya siasa Kata ni Jane Kitwala, Jacob Kasole na Lwaganwa Mganga huku mjumbe wa mkutano Mkuu Mkoa akichaguliwa kuwa Paul Marwa.

Wajumbe wa mkutano mkuu Kata ya Pamba ni Emmanuel Goroba, Frank Makuru, Willium Martin, Esther Joseph na Hassan Chaus ambapo wajumbe wa Halmashauri Kuu Kata ni Jane Kiale, Lwaganwa Mganga, Jacobo Kasole, Laurent Jicho na Frank Makuru.

Katibu wa CCM wilayani Nyamagana ambaye ndiye Mkurugenzi Mkuu wa Uchaguzi wilayani humo, Clemence Mkondya alisema chaguzi hizo zinaendelea vyema ambapo aliwataka wapiga kura kuendelea kusimamia haki katika chaguzi hizo wakipiga vita suala la rushwa.

Tazama video hapo chini

Wajumbe wa Mkutano Mkuu Kata ya Pamba Jijini Mwanza, wakimsikiliza Mwenyekiti Mteule wa CCM Kata hiyo, Ayoub Michael Oyubi baada ya kuchaguliwa kuwa mwenyekiti

Kutoka kushoto ni Katibu wa CCM Wilayani Nyamagana Clemence Mkondya, Mwenyekiti wa CCM Kata ya Pamba Ayoub Michael Oyugi, Msimamizi Msaidizi wa uchaguzi Charles Marwa Nyamasiriri pamoja na Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi Donata Yusuph Gapi

Florah Magabe ambaye ni mjumbe wa Mkutano Mkuu kutoka wilaya ya Nyamagana akitoa maoni yake kuhusiana na chaguzi za CCM zinazoendelea nchini

BMG Habari, Pamoja Daima!

Recommended for you