Audio & Video

DC Nyamagana akabidhi Bima za NHIF kwa madereva na Makondakta

on

Mwenyekiti wa MWAREDDA akipokea kadi ya matibabu kutoka NHIF kutoka kwa Mkuu wa Wilaya Nyamagana Mhe.Marry Tesha aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella kwenye uzinduzi wa Mpango wa utoaji Bima ya Afya kwa watumiaji wa vyombo vya moto wakiwemo madereva daladala, bodaboda na makondakta kupitia mpango wa KIKOA.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Mkuu wa Wilaya Nyamagana mkoani Mwanza Mhe.Marry Tesha leo amekabidhi kadi za bima ya afya kupitia mfuko wa NHIF kwa wanachama 36 wa Chama cha Madereva na Makondakta wa Daladala Mkoa wa Mwanza MWAREDDA.

Mhe.Tesha amekabidhi kadi hizo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella katika hafla fupi iliyofanyika Buzuruga Jijini Mwanza ambapo amewahimiza wajasiriamali wengine kupitia vikundi vyao kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya NHIF ili kunufaika na huduma bora za matibabu kwa gharama nafuu.

Ezekiel Lameck ambaye ni Mwenyekiti Msaidizi MWAREDDA amesema chama hicho kilianzishwa mwaka jana kikiwa na wanachama 50 ambapo hadi sasa kina wanachama 320 hivyo lengo ni kuhakikisha wanachama wote wanajiunga na mfuko wa NHIF ili kuondokana na adha ya kupata huduma za matibabu.

“Lengo la kuanzishwa kwa chama hiki ni kutetea haki na wajibu wa madereva na makondakta katika kazi zao, kutoa elimu na kuwajengea uwezo ili waweze kumudu vyema majukumu yao kwa mjibu wa sheria za nchi hususani sheria za usalama barabarani pamoja na kupigania mazingira bora ya kazi zao”. Amebainisha Lameck.

Naye Kaimu Meneja mfuko wa NHIF Mkoa wa Mwanza, Calystus Mpangala amesema kwa mwaka wa fedha 207/18 malengo yalikuwa kusajili wajasiriamali 1200 mkoani Mwanza kupitia mpango wa KIKOA ambapo hadi sasa umevuka lengo kwa kusajili wajasiriamali 1,223 hii ikiwa ni sawa na asilimia 102.

Mwenyekiti Msaidizi wa MWAREDDA, Ezekiel Lameck akipokea kadi ya matibabu kutoka NHIF kutoka kwa Mkuu wa Wilaya Nyamagana Mhe.Marry Tesha

Mwenyekiti Msaidizi wa MWAREDDA, Ezekiel Lameck akisoma risala kwenye hafla hiyo

Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Mhe.Marry Tesha akizungumza kwenye hafla hiyo

Mwakilishi wa Mbunge Jimbo la Nyamagana Ahmed Misanga (kulia), akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha Madereva na Makondakta wa Daladala Mkoa wa Mwanza MWAREDDA, Mjalifu Manyasi (kushoto)

SOMA Madereva wa serikali watoa ya moyoni

Recommended for you