Habari Picha

Wanafunzi chuo cha IFM Mwanza wakabidhi msaada kwa watoto wa FKT

on

Rais wa serikali ya wanafunzi wa chuo cha IFM tawi la Mwanza, Peter Kahindi (kushoto), akimkabidhi boksi la maziwa mwakilishi wa Kituo cha Foundation Karibu Tanzania FKT, Asunta Ngatunga (kulia).
Na Oscar Mihayo-BMG Habari
Uongozi wa serikali ya wanafunzi wa chuo cha usimamizi wa fedha IFM tawi la Mwanza, umekabidhi msaada wa mahitaji mbalimbali katika kituo cha kupiga vita ukatili wa watoto majumbani FKT.
Rais wa chuo hicho, Peter Kahindi anasema waliguswa na wahanga waliofangiwa matukio ya ukatili kwa kutoa walichonacho kama jitihada za kueneza elimu kwa jamii ili kuondokana na vitendo hivyo viovu.
Alitaja mahitaji waliyoyakabidhi kuwa ni pamoja na nguo, mchele, magodoro, sukari, sabuni, madaftari na kalamu yenye thamani ya shilingi Milioni tatu za kitanzania.
“Sisi wanafunzi tunatoa tulichobarikiwa na Mungu kwa watu wenye uhitaji ili kuwatia moyo na kujihisi wako pamoja na jamii licha ya kuwa kwenye msongo mkubwa wa mawazo”. AAlisema Kahindi.
Akipokea zawadi hizo, Asunta Ngatunga ambaye ni mwakilishi wa kituo hicho aliwashukuru wanafunzi hao kwa misaada huo kwa kusema imekuja wakati sahihi kutokana na watoto hao kuwa na mahitaji mengi.
Naye Lucy Hiza kutoka idara ya uokoaji IFM, alisema licha ya elimu kutolewa kwenye jamii, bado ukatili uko juu hivyo mahitaji kwa watoto hao bado ni changamoto na hivyo kuomba vyuo vingine kuiga mfano wa IFM.
Aidha Makamu wa Raisi IFM, Theofrida Ngonyani alisema wamekabidhi mahitaji mbalimbali katika Kituo cha afya Buzuruga na badae FKT lakini wanampango wa kuzungukia hospitali za wilaya, mkoa pamoja na Kituo cha kulelea wazee Bukumbi.

Baadhi ya mahitaji yaliyokabidhiwa kituoni hapo, juzi jumamosi Aprili 07,2018.

Recommended for you