Audio & Video

Wanafunzi wa chuo cha SAUT Mwanza kuadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani

on

Judith Ferdinand,  BMG

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. John Mongella anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani 2018 ambayo huadhimishwa Machi 8 kila mwaka.

Maadhimisho hayo ambayo yameandaliwa na Kikundi cha Wanafunzi Wanawake wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino SAUT Mwanza (SAUT STUDENTS WOMEN GROUP) ambapo yatafanyika katika ukumbi wa M10 kuanzia saa tatu asubuhi.

Akizungumza na BMG, Mshauri wa  Kikundi hicho, Joseph Badokufa alisema lengo ni kusherekea mafanikio ya wanawake pamoja na kuwatia moyo wanawake wengine kuwa wanaweza.

Badokufa alisema pia katika maadhimisho hayo wanawake na wanafunzi wa kike watapatiwa elimu ya namna ya kujikomboa kielimu na kiuchumi ili kuondokana na ukatili wa kijinsia.

Pia alisema itakuwa nafasi nzuri ya wanawake kujadili mbinu ambazo zitawasaidia kujitambua na kujikomboa ili kuleta usawa wa kijinsia katika masuala mbalimbali ikiwemo ya maendeleo.

Aliwaomba wakazi wa Jiji la Mwanza kujitokeza kwa wingi hasa wanawake kwani ni siku yao muhimu ya kujifunza mambo mbalimbali kwa manufaa yao.

Aidha alisema katika kuadhimisha siku hiyo, itaendana na shughuli mbalimbali ikiwemo, mashairi, ngoma za asili ya Afrika, hotuba, nyimbo, maonyesho ya mitindo kwa jinsia na mengine mengi.

Tazama HAPA Mjadala wa Wanamabadiliko mkoani Mwanza

Recommended for you