Audio & Video

Shirika la Amref latoa mafunzo kwa wanahabari mkoani Simiyu

on

Mwanahabari Happy Severine kutoka gazeti la Nipashe akichangia mada kwenye mafunzo kwa waandishi wa habari mkoani Simiyu yanayotolewa na shirika la Amref Health Afrika kuanzia kuanzia leo Julai 04, 2018 Mjini Bariadi.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Shirika la Amref Health Africa limetoa mafunzo kwa waandishi wa habari mkoani Simiyu ili kuwajengea uwezo katika kuandika vyema habari za afya.

Shirika hilo linatekeleza miradi mbalimbali ya kuboresha sekta ya afya mkoani humo ikiwemo mradi wa Uzazi Uzima unaolenga kutokomeza vifo vya mama na mtoto.

Afisa Mawasiliano na Uchechemuzi katika mradi wa Uzazi Uzima unaotekelezwa na shirika la Amref Health Africa, Nuru Ngailo pamoja na baadhi ya washiriki wamezungumza na BMG Online TV kuhusiana na mafunzo hayo yatayofikia tamati Julai 06, 2018 Mjini Bariani.

Afisa Mawasiliano na Uchechemuzi, mradi wa Uzazi Uzima kutoka Shirika la Amref Health Africa, Nuru Ngailo akiwasilisha mada kwenye mafunzo kwa waandishi wa habari mkoani Simiyu

Mafunzo hayo yanalenga kuwajea uwezo wanahabari kufanya kazi kwa welezi hususani kusaidia kufikisha elimu kuhusiana na miradi inayotekelezwa na shirika la Amref Health Africa katika mkoa wa Simiyu ikiwemo mradi wa Uzazi Uzima unaolenga kupunguza vifo vya mama na mtoto

Wakufunzi kutoka shirika la Amref, Nuru Ngailo (kushoto) ambaye ni Afisa Mawasiliano na Uchechemuzi mradi wa Uzazi Uzima pamoja na Sophia Kimaro ambaye ni Afisa Jinsia mradi wa Uzazi Uzima

Sophia Kimaro ambaye ni Afisa Jinsia mradi wa Uzazi Uzima unaotekelezwa na shirika la Amref mkoani Simiyu akiwasilisha mada kwenye mafunzo hayo

Mwanahabari Constantin Mathias kutoka gazeti la Uhuru (kushoto) akichangia mada kwenye mafunzo hayo

Mwanahabari Derrick Milton kutoka gazeti la Mtanzania akichangia mada kwenye mafunzo hayo

Belensi China kutoka ITV akichangia mada kwenye mafunzo hayo

Mmoja wa wakufunzi wa mafunzo hayo, Kenneth Simbeye ambaye pia ni Rais Mstaafu wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania UTPC akizungumza kwenye mafunzo hayo

Mkufunzi Solomon Missana ambaye ni Afisa Mradi Uzazi Uzima unaotekelezwa na shirika la Amref mkoani Simiyu akiwasilisha mada kwenye mafunzo hayo

May Mbelwa kutoka shirika la Amref Health Africa

Wanahabari washiriki wa mafunzo hayo

PIA SOMA Shirika la Amref lakabidhi Ambulance mpya mkoani Simiyu

Recommended for you