Habari Picha

Wananchi kuhudumiwa BURE Hospitali ya Bugando Jijini Mwanza

on

Na George Binagi

Wananchi jijini Mwanza wamehimizwa kujitokeza kwa wingi kwenye “Kongamano la Watoa Tiba kwa Vitendo”, litakalofanyika kwenye viwanja vya Hospitali ya Kanda Bugando kuanzia jumatano Novemba 29 hadi ijumaa Disemba Mosi mwaka huu, ili kupata huduma ya ushauri kuhusiana na matatizo mbalimbali ikiwemo magonjwa.

Hata hivyo huduma hiyo itatolewa kwa wananchi siku moja tu ambayo ni jumatano Novemba 29, ambapo watahudumiwa bure kuanzia majira ya asubuhi.

Akizungumza na BMG, Mratibu wa kongamano hilo Bi.Joyce Karawa amesema wananchi watapata huduma ya ushauri nasaha bure kuhusiana na mitindo ya kimaisha inayopelekee ulemavu wa kimwili na kiakili na pia namna ya kujiepusha.

“Tunatarajia kuwa na wataalaumu wa afya kutoka hospitali ya Taifa Muhimbili, hospitali ya Rufaa KCMC, hospitali ya magonjwa ya akili Mirembe pamoja na nyinginezo hivyo tunawasihi wananchi kujitokeza kwa wingi ili kunufaika na huduma hiyo bure”. Amesema Bi.Karawa.

Kongamano hilo limeandaliwa na Chama cha Watoa Tiba kwa Vitendo Tanzania (Tanzanian Occupational Therapists Association-TOTA), likiwa na kauli mbiu ihimizayo “Kutanua Wigo wa Huduma kwa Watu wenye Ulemavu, Kujenga Uhuru wa Kujitegemea” ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mhe.John Mongella.

Recommended for you