Audio & Video

Wananchi kunufaika na Kongamano la Watoa Tiba kwa Vitendo Jijini Mwanza

on

Kongamano la Watoa Tiba kwa Vitendo linatarajiwa kufanyika katika hospitali ya Rufaa Bugando Jijini Mwanza kuanzia kesho Novemba 29 hadi Disemba Mosi 2017.

Katika siku ya kwanza ya kongamano hilo ambayo ni kesho, wananchi watapatiwa huduma mbalimbali ikiwemo ushauri na matatizo ya kiafya yatokanayo na mtimo wa maisha na namna ya kuepukana nayo.

Kongamano hilo limeandaliwa na Chama cha Watoa Tiba kwa Vitendo Tanzania (Tanzanian Occupational Therapists Association-TOTA), na hapa Bi.Joyce Karawa ambaye ni Mtoa Tiba kwa Vitendo kutoka hospitali ya Bugando anafafanua zaidi.

Baadhi ya viongozi wa TOTA wakiwa na Mganga Mkuu mkoani Mwanza, Dkt.Leonard Subi (wa pili kulia), walipomtembelea ofisini kwake leo.

Bonyeza BMG Habari, Pamoja Daima kusoma zaidi

Bonyeza BMG Habari, Pamoja Daima kusoma zaidi

Recommended for you