Audio & Video

Watu 13 watia mbaroni mkoani Mwanza kwa amri ya Mkuu wa Wilaya

on

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Watu 13 wamekamatwa Jijini Mwanza kwa amri ya Mkuu wa wilaya Nyamagana Mhe.Marry Tesha baada ya kukuta wamefungua biashara zao wakati zoezi la usafi likiendelea.

Waliokamatwa kwa amri ya DC Tesha ni pamoja na wafanyabiashara ndogondogo (machinga) pamoja na Mama Lishe ambapo wamefikishwa kwa mwanasheria wa Jiji la Mwanza ili kukabiliana na sheria ambayo inaweza kuwa faini, kifungo ama vyote kwa pamoja.

Aidha Mhe.Tesha amemwagiza Kaimu Kamanda wa Polisi Nyamagana, Almachius Mchunguzi kumtia nguvuni Mtendaji wa Kata Mbugani, Benedict Kabadi pamoja na Watendaji sita wa Kata hiyo kwa kushindwa kusimamia vyema zoezi la usafi hii leo (Mei 26, 2018) jumamosi ya mwisho wa mwezi.

Kila jumamosi ya mwisho wa mwezi kuanzia saa moja hadi saa nne asubuhi ni siku maalum kwa ajili ya wananchi wote kushiriki zoezi la usafi nchi nzima ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan.

ISOME PIA HABARI HII Wasabato walalamika kupangiwa majukumu jumamosi

Recommended for you