Audio & Video

Wawekezaji wahofia Maji na Umeme wa Uhakika mkoani Mwanza

on

Judith Ferdinand, Mwanza

Serikali mkoani imehimizwa kuendelea kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo maji na umeme kwa wawekezaji ili kusaidia kufikia uchumi wa kati kupitia viwanda nchini.

Mkurugenzi wa kiwanda kinachijishughulisha na uzalishaji nyama cha Chobo Investiment kilichopo wilayni Misungwi, John Chobo aliyasema hayo wakati akizungumza na BMG  kwenye uzinduzi wa “Mwongozo wa Uwekezaji mkoani Mwanza”.

Chobo alisema wawekezaji mkoani Mwanza wanakabiliwa na tatizo la maji na umeme wa uhakika jambo ambalo hukwamisha utendaji mzuri wa shughuli za uzalishaji.

Alisema kiwanda hicho kina uwezo wa kusambaza nyama nchini nzima na hivyo kuiomba serikali iangalie namna ya kutatua changamoto za uwekezaji na kuwapa kipaumbele wawekezaji wa  ndani katika kukuza uchumi wa taifa.

“Wawekezaji mkoani Mwanza tunakabiliwa na uhaba wa maji na kutokua na umeme wa uhakika,ambao unapelekea uzalishaji kusimama, hivyo naiomba serikali itusaidie kutatua changamoto hiyo sambamba na kuwapa kipaumbele wawekezaji wa ndani,kwani tunauwezo wa kulisha nyama nchi nzima,” alisema Chobo.

Naye Mkurugenzi wa Chuo Kikuu Huria nchini tawi la Mwanza, Ancyfrida Prosper alisema wao ni wawekezaji katika elimu ambapo watazalisha wataalamu watakao kuwa wamejikita katika sayansi, ili waweze kusukuma gurudumu la viwanda na kutimiza malengo ya serikali kufikia uchumi wa kati ifikapo 2025.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mradi wa Kimataifa wa Maendeleo (UNDP) nchini  Tanzania,  Amon Manyama alisema serikali na UNDP wanajitahidi kupunguza taratibu zilizokuwa zinawachelewesha wawekezaji ili waweze kujitojeza katika fursa za kuwekeza Mwanza kwani ni mkoa ambao umekaa vizuri kwa kuzungukwa na nchi za ukanda wa Afrika Mashariki ambapo ni rahisi kufikia soko na kukuza uchumi wa nchi.

Hata hivyo Mtafiti wa  Taasisi ya Utafiti Uchumi na Jamii, Dkt. Bohela Lunogelo alisema mkoa huo una fursa za uwekezaji katika nyanja mbalimbali ikiwemo,uvuvi,mifugo,madini,michezo,ulimaji na usindikaji wa  matunda na mbogamboga kwa hekali 7000 zilizopo kwa ajili ya kilimo cha umwangiliaji.

Pia alisema kuna fursa ya uwekezaji wa machinjio ya kisasa kwani zaidi ya ngombe laki mbili wanachinjwa kila siku hivyo wakiwekeza watachinjwa zaidi sambamba na kunenepesha ng’ ombe na kuwauza kwenye viwanda.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella akizungumza kwenye uzinduzi huo.

Recommended for you