Audio & Video

Wazee Manispaa ya Ilemela sasa mambo safi

on

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, Renatus Mulunga akizungumza jana kwenye uzinduzi wa Baraza la Wazee Kata ya Mecco. Uzinduzi huo ulikwenda sanjari na kukabidhi vitambulisho vya msamaha wa matibabu kwa wazee wa Kata hiyo.

George Binagi-GB Pazzo @BMG

Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza imejipanga kuhakikisha inasimamia vyema sera ya matibabu bure kwa wazee.

Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, Dr.Florian Tinuga (kushoto), akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa Baraza la Wazee Kata ya Mecco pamoja na kukabidhi vitambulisho vya matibabu bure kwa wazee wa Kata hiyo.

Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, Dr.Florian Tinuga (kulia), akiteta jambo na Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Kata ya Mecco, Mzee Mohamed Yusuph.

Diwani wa Kata ya Mecco, Godlisten Kisanga akizungumza kwenye hafla hiyo.

Diwani wa Kata ya Mecco (katikati), Afisa Mtendaji wa Kata hiyo (kulia), wakiteta jambo na mmoja wa wazee baada ya hafla ya kuzindua Baraza la Wazee Kata ya Mecco pamoja na kukabidhi vitambulisho vya matibabu kwa wazee wa Kata hiyo. Bonyeza HAPA kwa habari zaidi ama bonyeza hapo chini. 

 

Recommended for you