Audio & Video

Mapokezi ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Jijini Mwanza

on

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa amewasili Jijini Mwanza na kupokelewa na viongozi mbalimbali wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa Mhe.John Mongella, majira ya saa nne asubuhi katika uwanja wa ndege wa Mwanza.

Waziri Majaliwa amewasili Jijini Mwanza kufungua rasmi mashindano ya umoja wa michezo kwa shule za sekondari nchini UMISETA ambayo yalianza kutimua vumbi tangu Juni 04, 2018 katika viwanja wa shule ya sekondari Nsumba pamoja na Chuo cha Ualimu Butimba.

Mashindano hayo yanatarajiwa kufikia tamati Juni 16, 2018 ambapo uzinduzi rasmi unafanyika katika uwanja wa CCM Kirumba hii leo jumamosi Juni 09, 2018.

Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa, akisalimiana na Mkuu wa Wilaya Magu ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa Wilaya Ilemela Mhe.Khadija Nyembo.

Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi Manispaa ya Ilemea, John Wanga

Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa akisalimiana na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela Renatus Mulunga

Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa akisalimiana na Afisa Elimu mkoani Mwanza, Mwl.Michael Ligola

Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mkoani Mwanza, Hellen Bogoya

Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa akisalimiana na Askofu Zenobius Issaya ambaye ni Mwenyekiti Mwenza wa Kamati ya Amani ya Viongozi wa Dini Mkoa Mwanza

Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa akisalimiana na Sheikh Hassan Kabeke ambaye ni Mwenyekiti Mwenza wa Kamati ya Amani ya Viongozi wa Dini Mkoa Mwanza

Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi wa CCM mkoani Mwanza

Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi wa kiwanda cha nyama, Chobo Inestiment

Ndege ya Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa ikiwasili uwanja wa ndege wa Mwanza

Recommended for you