Audio & Video

Waziri Mkuu aandaa Futari kwa viongozi mbalimbali mkoani Mwanza

on

Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa akizungumza kweny hafla ya futari ya pamoja na viongozi mbalimbali wakiwemo wa dini zote, vyama vya siasa, serikali pamoja na taasisi iliyofanyika jana Juni 09, 2018 katika viunga vya Chuo cha Benki Kuu, Capripoint Jijini Mwanza.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa dini zote kutokubali kugombanishwa na baadhi ya watu wasiolitakia mema taifa na badala yake waendelee kushirikiana ili kuimarisha amani nchini.

Waziri Mkuu Majaliwa alitoa rai hiyo jana wakati akizungumza kwenye hafla ya futari aliyoiandaa kwa viongozi wa viongozi na waumini wa dini za Kiislamu, Kikiristo na serikali iliyofanyika katika viunga vya Chuo cha Benki Kuu, Capripoint Jijini Mwanza.

Mhe.Majaliwa aliwahimiza viongozi wa dini zote kufanya kazi kwa misingi iliyowekwa na kwamba inapotokea jambo lolote haliko sawa walitatue kwa njia ya mazungumzo akisema serikali iko tayari kuendelea kushirikiana na dini zote.

Akizungumza kwa niaba ya Kamati ya Amani ya Viongozi wa Dini mkoani Mwanza, Askofu Charles Sekelwa alisema viongozi wa dini wataendelea kushirikiana na serikali kuimarisha umoja na mshikamano uliopo, akitoa pongezi kwa Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella kwa ushirikiano wake wa dhati.

Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella akitoa salamu zake kwenye hafla hiyo.

Naibu Wziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa OR-TAMISEMI, Mhe.Joseph Kakunda akitoa salamu zake kwenye hafla hiyo

Sheikh wa wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, Sheikh Athuman Ndaki akizungumza kwenye hafla hiyo

Mwenyekiti Mwenza wa Kamati ya Amani ya Viongozi wa Dini mkoani Mwanza Askofu Charles Sekelwa akitoa salamu kwa niaba ya kamati hiyo

Sheikh Hassan Kabeke ambaye ni Mwenyekiti Mwenza Kamati ya Amani ya Viongozi wa Dini mkoani Mwanza akakitoa mwongozo wa hafla hiyo ya Furari iliyoandaliwa na Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa

Sheikh Hassan Kabeke ambaye ni Mwenyekiti Mwenza Kamati ya Amani ya Viongozi wa Dini mkoani Mwanza akizungumza kwenye hafla hiyo

Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa (kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi wa kampuni ya mafuta MOIL, Altaf Mansoor (kulia) kwenye hafla hiyo

Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa akiwa kwenye hafla ya futari aliyoiandaa mkoani Mwanza

Viongozi mbalimbali wakiwemo wa dini zote, vyama vya siasa, serikali, mashirika, mahakama, Naibu Spika, wabunge, Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoa walishiriki hafla ya futari iliyoandaliwa na Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa mkoani Mwanza.

SOMA Mkurugenzi Ilemela atoa zawadi ya Mwezi Mtukufu kwa wenye uhitaji

Recommended for you