Habari Picha

Waziri wa OR-TAMISEMI kuwa mgeni rasmi Mkutano Mkuu wa TANNA

on

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhe Selemani Jafo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Mkutano wa Chama cha Wauguzi Tanzania (TANNA) unaoanza leo Oktoba 02 hadi 05, 2018 katika ukumbi wa  Chuo cha Mipanga Jijini Dodoma.

Hayo yamesemwa na Makamu wa Rais wa Chama hicho, Ibrahim Mgoo wakati akizungumzia mkutano huo na kubainisha kwamba 
mkutano huo umetanguliwa na utoaji wa huduma kwa jamii bila malipo zilizoanza Septemba 28, 2018 na kufuatiwa na Kongamano la Kisayansi kuanzia tarehe kesho Oktoba 02, 2018.

Zaidi ya wauguzi 1,000 wanatarajiwa kushiriki mkutano huo kutoka mikoa ya Tanzania Bara ambapo kaulimbiu NI “Wauguzi; Mbiu inayoongoza, Afya ni Haki ya Binadamu”.

Makamu Rais TANNA, Ibrahim Mgoo Wananchi wakipata huduma 
Mwananchi wa Dodoma akichangia damu
 Wananchi wakisubiri huduma
 Muuguzi akitoa huduma ya upimaji wa VVU
Mkazi wa Dodoma, Hyasinta Chuwa akimuonesha Muuguzi, Vivienne Mchilasi baadhi ya kazi zinazo tolewa na wagonjwa wa akili baada ya kupata nafuu
Afisa Muuguzi, Mtaalamu wa macho Hospitali ya Msumi Wilaya ya Chamwino Mkoa wa Dodoma, Gilbert Subeth  alimfanyia uchunnguzi wa macho mkazi wa Dodoma.
Imeandaliwa na Khamisi Mussa

Recommended for you