Audio & Video

Mkuu wa wilaya ya Nyamagana asisitiza matumizi ya nishati mbadala

on

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Mkuu wa wilaya Nyamagana Mhe.Marry Tesha amewahimiza wananchi kutumia nishati mbadala ikiwemo gesi pamoja na mkaa unaotengenezwa kwa malighafi kama mabaki ya uchafu lengo likiwa ni kuondokana uharibifu wa mazingira kutokana na ukataji miti ovyo.

Mhe.Tesha alitoa rai hiyo jana wakati akizungumza kwenye kongamano maalum la maadhimisho ya kilele cha Wiki ya Mazingira ambayo huadhimishwa Juni 05, kila mwaka lililofanyika kiwilaya katika ukumbi wa halmashauri ya Jiji la Mwanza.

Baadhi ya washiriki wa kongamano hilo pia walisisitiza wananchi kutunza mazingira ikiwemo kujiepusha na matumizi ya mifuko ya plastiki, uchafuzi wa vyanzo vya maji pamoja na ukataji ovyo wa miti.

SOMA Manispaa ya Ilemela yapanda miti kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani

Recommended for you