Audio & Video

Zahanati ya John Mongella yarahisisha huduma za afya kwa wananchi

on

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Wajumbe wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa Tanzania (ALAT) tawi la Mkoa wa Mwanza wametembelea zahanati ya John Mongella iliyopo katika Kijiji cha Bundilya wilaya Magu mkoani Mwanza na kuridhishwa na ujenzi wa zahanati hiyo.

Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya Magu, Lutengano Mwalwiba amesema ujenzi wa zahanati hiyo umegharimu shilingi milioni 54 ikiwa ni fedha za halmashauri, wananchi pamoja na wahisani.

Mmoja wa akina mama aliyefika katika zahanati hiyo kupata huduma amesema imewaondolea usumbufu wa kufuata huduma za afya umbali mrefu na hivyo kuomba serikali iendelee kuboresha huduma ikiwemo kuongeza watumishi wa afya pamoja na dawa.

Mwenyekiti wa ALAT mkoani Mwanza, Hilali Elisha ambaye pia ni Mwenyekiti halmashauri ya Magu amesema jambo kubwa la kujifunza katika halmashauri hiyo ni matumizi sahihi ya fedha kupitia utaratibu wa “Force Account” ambapo miradi mingi ya maendeleo ikiwemo afya, elimu na maji imetekelezwa vyema kwa gharama nafuu.

SOMA>>>Jumuiya ya ALAT Mwanza yaeleza ilichobaini halmashauri ya Misungwi

Recommended for you