Habari Picha

Zao la Mahindi wilayani Tarime

on

Msimu wa kilimo uliopita wilayani Tarime, bei ya mahindi ilipanda hadi kuuzwa kati ya shilingi 20,000 na 25,000 kwa debe moja wilayani hapa. Hii ni kutokana na mazao mengi ya chakula ikiwemo zao hili kuathiriwa na ukame ulioyakumba maeneo mengi nchini.

Lakini hivi sasa wakati tayari mahindi mapya yameanza kuingia sokoni ingawa kwa uchache, bei ya zao hili imeshuka hadi kufikia kati ya shilingi 1o,000 na 12,000 kwa debe moja, hii ikiashiria kwamba bei hiyi itaendelea kushuka katika kuelekea kwenye msimu wa mavuno na hali ya upatikanaji wa chakula itaendelea kukidhi mahitaji.

Rai ya BMG ni kwa maafisa kilimo kuendelea kuwa karibu na wakulima katika utayarishaji wa mashamba na upandaji wa mazao mbalimbali kwani msimu huu wa kilimo Tarime baadhi ya maeneo ikiwemo Kenyamanyori, mazao kama vile mahindi yameathiriwa na wadudu hivyo wakulima ambao hawakupata dawa sahihi mazao yao yamedumazwa na wadudu hao. Hii itasaidia upatikanaji wa chakula cha kutosha kwa mahitaji ya chakula cha familia biashara pia.

George Binagi, BMG alipotembelea shamba lake lililopo Kenyamanyori wilayani Tarime, jana.

Recommended for you