Audio & Video

Kamati ya Siasa yaridhishwa na utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo Misungwi

on

George Binagi-GB Pazzo @BMG

Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, imeridhishwa na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani humo ikiwemo elimu, afya, maji pamoja na miundombinu.

Ni baada ya jana Mei 05,2018 kamati hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Misungwi, Daud Gambadu kwa kuambatana na Mkuu wa wilaya Misungwi, Mkurugenzi Halmashauri ya Misungwi pamoja na Watendaji wa halmashauri hiyo kufanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo.

“Tumepita kujiridha na kuona ni jinsi gani miradi ya serikali inavyotekelezwa ambapo miradi yote tuliyopita tumeridhika na kuona kwamba shughuli za serikali zinakwenda sawa kuanzia sekta ya maji, afya na elimu”. Alisema Gambadu.

Mkuu wa wilaya Misungwi Juma Sweda alisema miradi ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM ya mwaka 2015/20 ambayo inaelekeza seriali kuboresha shughuli za maendeleo kwa wananchi.

“Sisi kama wasimamizi wa Ilani ya uchaguzi tumekuja kuwaonyesha yale wanayotuelekeza tufanye ikiwemo sekta ya afya, elimu pamoja na maji. Sasa niombe watendaji kuanzia ngazi ya Kijiji, Kata na Wilaya kila mtu ajitume na awajibike kwa kasi ya serikali ya awamu ya tano huku wananchi wakiendelea kuchangia nguvu kazi ili serikali ikamilishe miradi ya maendeleo”. Alisisitiza Mkurugenzi halmashauri ya Misungwi Eliurd Mwaiteleke.

Kamati hiyo ilikagua miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa wodi ya upasuaji katika kituo cha afya Mbarika, tanki la maji Kijiji cha Lutalutale, chanzo cha maji KASHWASA, shule ya sekondari Gulumungu, madarasa shule ya msingi Buhingo, nyumba ya waalimu Isakamawe, madara shule ya sekondari Misasi, ujenzi wa wodi ya akina mama kituo cha afya Misasi, shule ya sekondari Aimee Milembe, shule ya sekondari Paul Bomani, maadara ya elimu maalumu shule ya msingi Busagala, ujenzi wa shule ya msingi Isela pamoja na ujenzi wa zahanati ya Kijiji cha Ngeleka.

Ukaguzi wa wodi ya upasuaji katika kituo cha afya Kata ya Mbarika.

Ukaguzi wa tenki la maji Kijiji cha Lutalutale.

Ukaguzi wa miundombinu ya maji (mtandao wa mabomba), mradi wa maji Ngaya-Mbarika.

Uunganishaji mabomba kwenye mradi wa maji Ngaya-Mbarika.

Ukaguzi wa chanzo cha maji KASHWASA.

Kaimu Mkuu wa kituo cha KASWASA, Cheyo Kanuda (wa pili kulia), akimsikila Mkurugenzi halmashauri ya Misungwi (kulia). Wengine ni viongozi na wajumbe wa Kamati ya Siasa wilaya ya Misungwi.

Chanzo cha maji KASHWASA.

Ukaguzi wa shule ya sekondari Galumungu Kaya ya Galumungu inayojengwa kwa nguvu za wananchi.

Ukaguzi wa shule ya sekondari Galumungu Kaya ya Galumungu inayojengwa kwa nguvu za wananchi.

Ukaguzi wa madarasa matatu shule ya msingi Buhingo Kata ya Buhingo.

Mkuu wa wilaya Misungwi, Juma Sweda akikagua uezekaji madarasa ya shule ya msingi Buhingo.

Mjumbe wa Kamati ya Siasa wilayani Misungwi akishiriki ujenzi wa madarasa shule ya msingi Buhingo.

Kamati ya siasa wilayani Misungwi ikisikiliza taarifa kutoka kwa Afisa Elimu msingi wilayani Misungwi, Mwl.Ephraim Majinge.

Ujenzi wa nyumba ya waalimu (Six in One) katika shule ya Isakamawe Kata ya Kijima.

Mhandisi Sudy Khamis akitoa taarifa ya ujenzi wa nyumba ya waalimu shule ya Isakamawe kwa Kamati ya Siasa wilayani Misungwi.

Ukaguzi wa madarasa matatu katika shule ya sekondari Misasi yanayokusudiwa kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha tano na sita na madarasa hayo yanajengwa kwa nguvu za wananchi na serikali.

Ukaguzi wodi ya wazazi kituo cha afya Misasi.

Ukaguzi ujenzi wa daraja barabara ya Lubuga.

Ukaguzi maabara za shule ya sekondari Aimee Milembe Kata ya Misungwi.

Vyoo bora shule ya sekondari Aimee Milembe.

Nyumba ya mantroni shule ya sekondari Aimee Milembe.

Ukaguzi madarasa shule ya sekondari Paul Bomani.

Ukaguzi nyumba ya walimu shule ya sekondari Paul Bomani.

Ukaguzi wa vyoo shule ya msingi Busagala.

Ukaguzi wa madarasa shule ya msingi Isela baada ya kugawanyika kutoka shule ya msingi Busagala.

Ukaguzi vyoo shule ya msingi Isela.

Ukaguzi barabara ya Nyashishi-Ngeleka-Fella baada ya barabara hiyo kuharibika kutokana na mvua.

Ukaguzi Zahanati ya Kijiji cha Ngeleka.

Tazama video kutoka BMG Habari hapa chini.

Bonyeza BMG Habari ama BMG kwa habari zaidi kutoka Misungwi

Recommended for you