Habari Picha

Wananchi jimbo la Ilemela wapongezwa na mbunge wao

on

Judith Ferdinand,BMG

Mbunge wa jimbo la Ilemela mkoani Mwanza Mhe.Dkt.Angeline Mabula ameendelea na ziara yake ya kukagua utekelezaji miradi mbalimbali ya maendeleo jimbo humo ili kujionea namna Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015/20 ya Chama cha Mapinduzi CCM inavyotekelezwa.

Akiwa katika Kata ya Sangabuye jana, Mhe.Dkt.Mabula ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi aliwapongeza wananchi wa Kata hiyo kwa namna wanavyoshiriki utekelezaji wa miradi mbalimbali za maendeleo ikiwemo afya na elimu.

“Maendeleo yanaletwa kwa ushirikiano wa mafiga matatu ambayo ni jamii, Halmashauri na mbunge nawasihi muendelee kuchangia shughuli mbalimbali za maendeleo nasi tutawaunga mkoni”. Alisisitiza Mhe.Dkt.Mabula.

Akitoa taarifa kwa Dkt.Mabula wakati akikagua ujenzi wa shule ya msingi Ihalalo, Mratibu wa Mradi wa Makazi Bora wa Halmashauri hiyo Yusuph Omollo alisema ujenzi huo umekamilika kwa asilimia 99 hivyo mwaka shule hiyo itafunguliwa

Alisema ujenzi wa shule hiyo ulianza kwa nguvu za wananchi, Halmashauri na wafadhili ambapo yanajengwa madarasa matatu tangu mwezi Februari mwaka huu kwa gharama za shilingi milioni 92.94, wananchi wakichangia milioni 3.75, Halmashauri milioni 35.19 zilizoplipa fidia ya eneo lenye ukubwa wa heka 5.9 na wafadhili kutoka nchini Korea Kusini milioni 54.

Recommended for you