Habari Picha

Mbunge jimbo la Ilemela aanza ziara kukagua miradi ya maendeleo

on

Judith Ferdinand, BMG

Mbunge wa Jimbo la Ilemela ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt.Angeline Mabula ametoa rai kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela John Wanga kwa kushirikiana na madiwani wa Kata ya Nyamhongolo na Buswelu kuhakikisha bonde la Nyamadoke haliharibiwi kutokana na shughuli za kibinadamu.

Dkt Mabula alitoa rai hiyo jana alipofanya alipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa zahanati ya Nyamadoke sambamba na kuzungumza na wananchi ikiwa ni mwanzo wa ziara yake ya siku tano katika jimbo lake.

“Mkurugenzi kwa kushirikiana na madiwani hususani Kata za Nyamhongolo na Buswelu msimamie vyema bonde hili ikiwemo kuzuia ujenzi kwani ni kinyume cha sheria ya ardhi na ndio maana kwenye upimaji shirikishi eneo hilo halijahusishwa na watu wasipoteze fedha zao katika kujenga eneo hilo kwani watakuja kuondolewa”. Alisema Dkt. Mabula.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa Kata ya Nyamhongolo Victor Leonard alisema mradi wa ujenzi wa zahanati ya Nyamadoke ulianza  Agosti 2013 hadi  Januari 2014  kwa nguvu za wananchi na fedha kutoka Serikali Kuu ukigharimu shilingi milioni 17.5.

Mbunge jimbo la Ilemela, Mhe.Dkt.Angeline Mabula (wa pili kushoto) pamoja na viongozi mbalimbali akiwemo Kaimu Mkuu wa Wilaya Ilemela Mhe.Khadija Nyembo (kushoto) walipofika Mtaa wa Nyamadoke kusikiliza kero mbalimbali za wananchi

Wananchi waliojitokeza kwa wingi kuongea na mbune wao

Recommended for you