Audio & Video

Jumuiya ya ALAT Mwanza yaeleza ilichobaini halmashauri ya Misungwi

on

Na George Binagi-GB Pazz, BMG

Jumuiya ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tanzania ALAT tawi la mkoa Mwanza imetoa pongezi kwa halmashauri ya wilaya Misungwi kwa usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo.

Mwenyekiti wa jumuiya hiyo Hilal Elisha alitoa pongezi hizo jana kwenye ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo elimu, afya na maji.

Katika ziara hiyo, jumuiya ya ALAT mkoani Mwanza ilitoa shilingi milioni mbili ili kusaidia ujenzi wa shule ya Sekondari Kata ya Gulumungu inayojengwa kwa nguvu za wananchi na halmashauri ambapo inatarajiwa kufunguliwa mwezi ujao ili kuwaondoa usumbufu wanafunzi wa Kata hiyo wanaotembea urefu wa kilomita 14 hadi Kata jirani ya Busongo.

Mkurugenzi halmashauri ya Misungwi, Eliurd Mwaiteleke alisema hatua hiyo inatokana na usimamizi bora wa fedha za miradi pamoja na utayari wa wananchi kuchangia shughuli za maendeleo.

Leo Juni 13, 2018 jumuiya ya ALAT mkoa Mwanza inahitimisha shughuli zake wilayani Misungwi kwa kufanya mkutano wa tathmini.

Mwenyekiti wa ALAT mkoani Mwanza, Hilal Elisha akizungumza na wanahabari

Mkurugenzi halmashauri ya Misungwi, Eliurd Mwaiteleke akifafanua jambo kwa wanahabari

Afisa Mipango halmashauri ya wilaya ya Misungwi, Sylivia Rwehabura akizungumzia utekelezaji wa miradi katika halmashauri hiyo.

Jumuiya ya ALAT mkoani Mwanza ikikagua jengo la utawala shule ya sekondari Gulumungu inayojengwa kwa nguvu za wananchi

Jumuiya ya ALAT mkoani Mwanza ikikagua ujenzi wa nyumba ya waalimu (6 in I) katika shule ya Sekondari Isakamawe

Ujenzi wa jengo la upasuaji katika Kituo cha Afya Mbarika unaendelea kwa kasi

Maabara katika shule ya Sekondari Aimee Milembe

Ujengo wa madarasa kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha tano na sita katika shule ya sekondari Misasi

Ujenzi wa madarasa matatu katika shule ya Msingi Buhingo

Ujenzi wa jengo la upasuaji katika Kituo cha Afya Misasi

Jumuiya ya ALAT mkoani Mwanza ikikabidhi mchele kilo 100 uliotolewa na Mkurugenzi wa halmashauri ya Ilemela pamoja na fedha kwa ajili ya mboga (mbuzi) shilingi laki mbili na elfu tatu katika shule ya Msingi Maalum Mitindo

Tazama picha mbalimbali za ziara hiyo

SOMA Jumuiya ya ALAT Mwanza yavutiwa na miradi ya maendeleo wilayani Sengerema

Recommended for you