Audio & Video

Mongella aeleza ni kwa nini Rais Magufuli anastahili mapokezi makubwa

on

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli anatarajiwa kufanya ziara ya kikazi mkoani Mwanza jumatatu Septemba 03- 04, 2018.

Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe. John Mongella amesema kesho Septemba 03, 2018 Mhe. Rais Dkt. Magufuli atashuhudia utiaji saini mikataba ya ujenzi wa meli mpya, chelezo na ukarabati wa meli za MV. Victoria na MV. Butiama ambapo hafla hiyo itafanyika katika eneo la Bandari ya Mwanza Kusini kuanzia majira ya saa moja asubuhi.

Amesema jumanne Septemba 04, 2018 majira ya saa mbili asubuhi, Mhe. Rais Dkt. Magufuli atazindua kiwanda cha Lakairo Group of Companies kilichopo Kijiji cha Isangijo wilayani Magu, majira ya saa sita atazindua mradi wa upanuzi wa Chuo cha Ualimu Murutunguru wilayani Ukerewe.

Siku hiyo hiyo majira ya saa nane mchana Mhe. Rais Dkt. Magufuli atazindua mradi wa maji katika Kijiji cha Nebuye wilayani ukerewe na majira ya saa tisa mchana atazungumza na wananchi kupita mkutano wa hadhara utakaofanyika katika uwanja wa Getrude Mongella uliopo Nansio.

Mhe. Mongella amewahimiza wananchi wote kujitokeza kwa wingi kumlaki Mhe. Rais Dkt. Magufuli katika maeneo yote atakayopita kutokana na nia yake ya dhati katika kuiletea Tanzania maendeleo.

PIA SOMA Ratiba na shughuli atakazofanya Rais Magufu mkoani Mwanza

Recommended for you