Habari Picha

WABUNGE WASIMAMA KWA MUDA BUNGENI.

on

Bunge limezizima kwa makofi baada ya hotuba ya mpango wa bajeti ya kambi rasmi ya upinzani.Wabunge wa upinzani ndiyo wengi waliobaki ukumbini baada ya wengi kwenda kufuatilia ripoti ya kamati ya pili ya Rais John Magufuli kuhusu usafirishaji wa makinikia.
Wabunge wamesimama na kuanza kuimba huku wakipiga makofi, marais wa awamu zilizopita; Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete wametajwa.

“Tuna imani na Mkaaapa…oya oya oya
Mkapa kweeeli…kweli
Kweli, kweli, kweli Mkapa.

Tuna imani na Kikweeetee…oya oya oya
Kikwete kweeli
Kweli, kweli, kweli Kikwete.”

Wimbo huo umeimbwa baada ya Waziri Kivuli wa Fedha na Mipango, David Silinde kulitaka Serikali kuileta bungeni mikataba yote ya madini ili ijadiliwe.

#BMGMtandaoni