Habari Picha

KIWANGO CHA RAIS MAGUFULI KUKUBALIKA CHAPOROMOKA.

on

Asilimia 71 ya watanzania wameeleza kuukubali utendaji kazi wa Rais John Pombe Magufuli tangu alipoingia madarakani mwaka 2015.

Hata hivyo kiwango hicho kimeshuka kutoka asilimia 96 mwezi juni mwaka jana licha ya kwamba kiwango cha Rais kukubalika kimetofautiana kulingana na makundi mbalimbali.

Asilimia 68 ya wenye umri chini ya miaka 30 wamesema wanamkubali Rais ikilinganishwa na asilimia 82 ya wenye umri wa zaidi ya miaka 50.

Asilimia 75 ya wananchi wenye elimu ya msingi au chini yake wamesema wanamkubali Rais ikilinganishwa na asilimia 63 ya wale wenye elimu ya sekondari au zaidi.

Asilimia 75 ya wananchi masikini wamesema wanamkubali Rais ikilinganishwa na asilimia 66 ya wananchi matajiri.

Wakati huo huo kukubalika kwa utendaji wa wabunge kumeshuka kutoka asilimia 79 mwezi juni mwaka jana hadi asilimia 58 mwezi Aprili mwaka huu.

Pia kukubalika kwa utendaji wa madiwani nchini kumeshuka kutoka asilimia 74 mwezi Juni mwaka jana hadi asilimia 59 mwezi Aprili mwaka huu.

Nako kukubalika kwa utendaji wa wenyeviti wa vijiji na mitaa nchini kumeshuka kutoka asilimia 78 mwezi Juni mwaka jana hadi asilimia 66 mwezi Aprili mwaka huu.

Matokeo hayo yametolewa hii leo na taasisi ya Twaweza katika utafiti wake uitwao matarajio, matokeo, vipaumbele, utendaji na siasa nchini tanzania.

Recommended for you