Habari Picha

MOTO WASABABISHA MAAFA NYUMBA YA KULALA WAGENI JIJINI MWANZA.

on

Moto umezuka katika nyumba ya kulala wageni, iitwayo Shinyanga Guest, katikati ya Jiji la Mwanza na kusababisha madhara ikiwemo mmiliki wa nyumba hiyo, Mzee Maduhu Shinyanga, kupoteza maisha.

Tukio hilo lilitokea jana majira ya saa moja jioni na inasemekana chanzo chake ni hitilafu ya umeme. Bado gharama halisi ya hasara hazijafahamika ambapo baadhi ya madhara makubwa yalitokea licha ya juhudi za jeshi la zima moto katika kupambana na moto huo.