Audio & Video

WENYE SIFA ZA KUCHANGIA DAMU.

on

Wananchi mkoani Mwanza wametakiwa kujenga utamaduni wa kuchangia damu mara kwa mara ili kuokoa maisha ya wagonjwa wenye uhitaji wa damu.

Afisa Mhamasishaji wa benki ya damu salama Kanda ya Ziwa, Bernadino Medaa, ameyasema hayo wakati akizungumza na Lake Fm katika kuelekea kwenye maadhimisho ya siku ya kuchangia damu duniani.

Maadhimisho ya siku ya kuchangia damu duniani yatafanyika juni 14 ambapo kwa mkoa wa Mwanza yanatarajiwa kufanyika katika viunga vya ofisi za benki ya damu Bugando Jijini Mwanza, lengo ikiwa ni kutambua mchango wa wachangiaji damu duniani. Tazama video hapo chini

Recommended for you