Habari Picha

SIKILIZA WIMBO MPYA KUTOKA KWAO JERUSALEM CITY SINGERS-HAJAKUSAHAU

on


SIKILIZA WIMBO KUTOKA KWAO JERUSALEM CITY SINGERS-HAJAKUSAHAU HAPA CHINI.

Mwanadamu unaweza kupitia majaribu na maswaibu mbalimbali katika hii dunia. Katika hayo maswaibu na majaribu unaweza kujikuta ukidhania hakuna tena msaada kutoka pahala popote pale. Hii inatokana na kupitia shida na matatizo mengi yanayopelekea kujiona uko peke yako katika ulimwengu huu.

Lakini pia hata pale unapokaribia kupata Faraja na msaada kutoka kwa mwanadamu mwenzako, majaribu na matatizo yanaweza kukung’ang’ania zaidi na hatimae hiyoa Faraja na msaada vyote kwa pamoja ukavikosa na kujikuta ukipoteza matumaini tena.
Na hapo ndipo Muumba wako anapochukua nafasi yake na kukutendea muujiza mpya na wa ajabu na kujikuta ukiamini kwamba kumbe ni kweli Mungu yupo na anaishi. Kutokana na hali hiyo unajikuta ukijisemea Moyoni “kumbe Mungu wangu hakunisahau wakati napitia majaribu na maswaibu katika hii dunia”.
Hivyo ndivyo ambavyo waimbaji wa Kwaya ya JERUSALEM CITY SINGERS kutoka Bugarika Jijini Mwanza wanavyokuletea Faraja kutoka kwa Mwenyezi Mungu wewe mwanadamu ambae upo katika matatizo mbalimbali hapa duniani ambapo Faraja yao inatoka katika Wimbo wao uliobeba Albamu yao ambayo inakwenda kwa jina la “HAJAKUSAHAU”.
Albamu hiyo yenye nyimbo 10 bora imejaa Baraka tele huku ikiwa na mchanganyiko wa Nyimbo mbalimbali za Injili ambazo zimegusa kila kona ya maisha yako. Nyimbo zinazopatikana katika hiyo Albamu ni Tembea na Yesu, Nikupe habari, Hajakusahau (Wimbo uliobeba Albam), Hii ndiyo habari, Ahsante, Nyakati za Hatari, Utatu Mtakatifu, Mungu wa Ajabu, Ilisikika Sauti pamoja na Kwa Rehema za Mungu.
Mwenyekiti wa Kwaya hiyo ya Jerusalem Bw.Samwel Maneno anasema kuwa Kwaya hiyo ambayo inaundwa na Waimbaji 13 waliobarikiwa na Mwenyezi Mungu katika huduma ya Uimbaji, imelenga kuleta tumaini jipya kwa kila mmoja anaepata fursa ya kusikiliza nyimbo zao za Injili.
Maneno anasema kuwa Uzinduzi wa Albamu ya Hajakusahau unatarajiwa kufanyika hivi karibuni Jijini Mwanza, hivyo wakati uzinduzi huo unasubiriwa kwa hamu kubwa ni vyema kwa yeyote mwenye kuhitaji nakala ya Albamu hiyo akapiga nambari 0758 061 044 au 0763 185 898 ili akajipatia nakala yake.

Hakika Usikubali kukosa nakala yako ya Albamu ya HAJAKUSAHAU kutoka kwao Jerusalem City Singers kutoka Bugarika Jijini Mwanza, kwa maana ni Albamu iliyojaa Faraja ya Kweli ambayo inatoka kwa Mwenyezi Mungu kupitia kwa Waimbaji wake aliowateua ili kuifikisha Faraja hiyo kwako popote pale ulipo.
Na:George Binagi-GB Pazzo

Recommended for you