Habari Picha

MAADHIMISHO YA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA 2017 MKOANI MWANZA.

on

Shirika la watoto la Railway Children Africa limefanikiwa kuwarejesha majumbani zaidi ya watoto 200 waliokuwa wakiishi mitaani jijini Mwanza.

Afisa Uhusiano wa shirika hilo, Aneth Isaya (pichani juu) ameyasema hayo kwenye maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika 2017 ambayo kwa mkoa wa Mwanza yamefanyika katika uwanja wa Furahisha.

“Shughuli yetu kubwa ni kuwaunganisha watoto waishio mitaani na familia zao maana yakiendelea kukaa mitaani wanapata madhara mengi yakiwemo ya kingono”. Amesema Isaya.

Naye meneja wa Kituo cha Huduma ya Mtoto cha EAGT Lumala Mpya jijini mwanza, Jorum Samwel amesema jamii pamoja na mashirika mbalimbali yanapaswa kuwalea watoto katika misingi bora ili kutimiza ndoto zao za baadaye.

Watoto mkoani Mwanza wametumia Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika 2017 kupaza sauti zao kupinga vitendo vya ukatili na unyanyasi kama anavyohimiza mtoto Neema Daniel kutoka shirika la WoteSawa.

Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yalitokana na azimio lililopitishwa na uliokuwa umoja wa nchi huru za Afrika oau mwaka 1990 kwa lengo la kuwakumbuka watoto wa kitongoji cha Soweto nchini  Afrika Kusini waliouawa juni 16 mwaka 1976 wakiandamana kudai haki ya kupata elimu bila ubaguzi.

Champion Esther Mtete kutoka Kata ya Buzuruga jijini Mwanza akieleza namna ambavyo amekuwa akishirikiana na shirika la Railway Chilredn Africa kuwarejesha makwao watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi.

Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Dkt.Leonard Masalle, kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella.

Wageni mbalimbali meza kuu

Madhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika 2017 uwanja wa Furahisha mkoani Mwanza

Mshereheshaji, George Kusekwa kutoka Baraza la Watoto mkoani Mwanza

Mshereheshaji, Halleluyah Benjamin kutoka Baraza la Watoto mkoani Mwanza

Watoto kutoka Kituo cha Huduma ya Mtoto cha Compassion 670 EAGT Lumala Mpya

Banda la shirika la WoteSawa la kutoa elimu na vipeperushi mbalimbali

Renalda Mambo ambaye ni Afisa Ustawi wa Jamii, Shirika la WoteDawa, akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika 2017

Mmoja wa watoto wafanyakazi wa nyumbani jijini Mwanza, Neema Daniel akizungumzia Siku ya Mtoto wa Afrika katika kutokomeza ukatili kwa watoto

Mkurugenzi wa Shirika la Kutetea Haki za Watoto Wafanyanyakazi wa Nyumbani WoteSawa, Angel Benedicto, amesema ingawa Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika hufanyika sambana na yale ya kupinga utumikishwaji wa watoto, lakini bado iko haja ya kuhakikisha serikali na wadau wengine wanaadhimisha Siku ya Kupinga utumikishwaji wa Watoto kila Juni 12.

Mwanafunzi kutoka Kituo cha Huduma ya Mtoto EAGT Lumala Mpya, akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika 2017 katika viwanja vya Furahisha

Jorum Samwel kutoka Kituo cha Huduma ya Mtoto EAGT Lumala Mpya jijini Mwanza, akizungumzia Siku ya Mtoto wa Afrika 2017

Champion Kamgisha Daniel akieleza namna ambavyo amekuwa akishirikiana na shirika la Railway Chilredn Africa kuwarejesha makwao watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi jijini Mwanza.

Recommended for you