Habari Picha

MAADHIMISHO YA SIKU YA KUONGEZA UELEWA KUHUSU UALIBINO 2017.

on

Chama cha watu wenye ualibino mkoani Mwanza TAS, kimeeleza dhamira yake ya kuhakikisha kwamba kinatokomeza aina zote za ubaguzi na ukatili kwa wenye ualibino.

Mwenyekiti wa chama hicho, Alfred Kapole (katikati) ameyasema wakati tanzania hii leo imeungana na mataifa mbalimbali duniani kuadhimisha siku ya kuongeza uelewa kuhusu ualibino.

Kapole alisema suala la kuondoa unyanyapaa pamoja na ukatili kwa watu wenye ualibino linawezekana, ikiwa kila mmoja katika jamii atawajibika kuimarisha ulinzi kwa watu wenye ualibino.

Mkoa wa Mwanza ni miongoni mwa mikoa yenye rekodi mbaya za matukio ya kutekwa, kukatwa viungo na kuuawa kwa watu wenye ualibino hapa nchini ambapo kuna takribani kesi 27 zilizoripotiwa mahakamani kutokana na vitendo hivyo.

Kitaifa Maadhimisho ya siku ya kuongeza uelewa kuhusu ualibino yamefanyika mkoani Dodoma, yakilenga kutoa elimu kuhusu ualibino na hatimaye jamii kuondokana na imani potofu ikiwemo kuhusisha viungo vya wenye ualibino na ushirikina.

Recommended for you