Habari Picha

KUHUSU WAKAZI WA NYAMONGO KUVAMIA MGODI WA NORTH MARA

on

Zaidi ya wananchi 300 kutoka maeneo mbalimbali ya wilaya ya Tarime mkoani Mara, wamevamia mgodi wa dhahabu wa North Mara Nyamongo wilayani humo wakishinikiza mamlaka za mgodi huo kuwalipa fedha zao za fidia kutokana na kutakiwa kupisha eneo la mgodi kwa ajili ya shughuli za uchimbaji.

Baadhi ya wananchi hao wamesema wamechukua hatua hiyo baada ya kukuta majina yao hayamo kwenye orodha ya wanaostahili kulipwa fidia katika tathmini waliyofanyiwa mwaka 2014.

Hata hivyo polisi wa kutuliza ghasia wamewadhibiti wananchi hao na hivyo kushindwa kuingia ndani ya mgodi, amesema Kamanda wa polisi mkoa wa kipolisi wa Tarime/Rorya, Andrew Sata.

Wananchi wa vijiji vinavyozunguka eneo la mgodi huo wameeleza kwamba kero sugu inayowasibu ni ucheleweshaji wa malipo ya fidia za za maeneo yao yaliyofanyiwa tathmini ili wamiliki husika wahame kupisha shughuli za mgodi.

Recommended for you