Audio & Video

WALIOISHI KWENYE MAHEMA MIAKA 10 GEITA, WAHAMIA NYUMBA WALIZOJENGEWA

on

BMG Habari tumepokea taarifa kwamba wale akina mama watatu waliokuwa wakiishi kwenye mahema tangu mwaka 2007 baada ya kuhamishwa kwenye maeneo yao ili kupisha kushughuli za uchimbaji wa dhahabu mkoani Geita, wamekubali kuhamia kwenye nyumba walizojengewa katika eneo la Buhalala mkoani Geita.

Wananchi wenzao waliohamishwa kutoka eneo la Mine Mpya kwenda eneo la Sophia Town kwa muda ili kupisha shughuli za mwekezaji, walikubali kuhamia kwenye nyumba walizojengewa lakini akina mama hawa watatu wao waligoma kuondoka.

Awali akina mama hawa walikataa kuhamia kwenye nyumba mpya walizojengewa wakishinikiza kupewa fidia ya pesa badala ya nyumba, lakini hatimaye jana Julai 27,2017 wamekubali kuhamia kwenye makazi hayo mapya waliyojengewa.

Taarifa ya kuhama kwao itakujia hapa hapa BMG Habari, kwa sasa tazama simulizi yao wakiwa kwenye mahema kabla ya kuhama ikiwa ni mahojiano waliyofanya na BMG Julai 03,2017.

Recommended for you